Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Jumuiya ya Waislamu ya Khoja Shia Ithanasheri imefanya matembezi ya kuomboleza kifo cha mjukuu wa Mtume Muhammad (saww), Imam Hussain (as) aliyeuawa miaka 1,300 iliyopita katika Mji wa Karbala nchini Iraq.
Matembezi hayo ambayo yanayojulikana kwa jina la SIKU YA ASHURA yamefanyika leo Julai 5,2025 kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
ASHURA ni siku ya kumi ya mwezi mtukufu wa Muharram. Katika siku hii ya Ashura mjukuu wa Mtume yaani Imam Hussain (as) aliuawa katika tambarare za mji wa Karbala baada ya kusimama kidete dhidi ya mtawala dhalimu wa wakati ule, Yazid bin Muawiya, akatoa fundisho la kukataa kumpigia magoti mdhalimu huyo, ndipo akajitolea maisha yake, akauawa ili kunusuru ubinaadamu , utu pamoja na kupigania uislamu.
Aidha, katika matembezi hayo, viongozi mbalimbali wa Dini na Siasa wamepata fursa kushiriki akiwemo Naibu Spika ambaye pia ni Mbunge wa Ilala, Mhe. Mussa Azzan Zungu, Mbunge wa Kinondoni, Abbas Tarimba, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Khoja Shia, Ndugu Mohamed Raza Dewji na Sheikh Mkuu wa TIC, Hemed Jalala.
Your Comment